COVID-19 Digital Classroom: Course Series (Swahili)

COVID-19 Digital Classroom: Course Series (Swahili)

Track Overview

Msururu wa kozi ya COVID-19 ni sehemu ya mkakati COVID-19 Digital Classroom. Kozi hizi zimeundwa kimsingi kwa wahudumu wa afya katika jamii wanaohudumu katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati. Inashughulikia mada mbalimbali kuhusu COVID-19, zikiwemo habari ya kimsingi juu ya virusi na jinsi ya kupunguza athari zake kwa afya ya umma. Kozi hii imeundwa kusanikisha habari muhimu zaidi, ya kiwango cha juu juu ya COVID-19 kutoka kwa rasilimali mbalimbali zinazoheshimiwa kwa njia ya vitendo. Rasilimali nyingi zimetajwa kwa marejeleo yako na zinajumuisha nyaraka na miongozo kutoka Shirika la Afya Duniani, Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, Chuo cha Afya ya Umma cha Johns Hopkins Bloomberg, Umoja wa Mataifa, na vyanzo vingine vingi vya kuaminika. Huku wahudumu wa afya katika jamii ndiyo hadhira ya msingi ya msururu huu wa kozi, mada zinazozungumziwa ni muhimu kwa kila mtu anayehusika katika kukabiliana na janga hili ulimwenguni.

Ni muhimu kutambua kwamba wakati kozi hizi zinatoa muhtasari wa jumla wa COVID-19 na habari juu ya jinsi ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu, haiwezi kushughulikia kila kitu, hasa kwani bado tunajifunza kila siku kuhusu virusi hivi na athari zake kwa afya na jamii.. Kwa hivyo, tafadhali tumia kozi hii kama mwongozo, na uendelee kujitambulisha na muktadha wako, pamoja na miongozo ya afya ya umma ya nchi yako, ili uweze kubadilisha yaliyomo tunayoshughulikia hapa kwa ajili yako na mahitaji maalum ya jamii yako.

Jiunge na Kundi la Facebook (Facegroup Group) kushirikiana na jamii ya wahudumu wa afya na viongozi wa afya ulimwenguni kwa kutumia makala ya COVID-19 Digital Classroom..

Covid Course 5 (Swahili)
Covid Course 5 (Swahili)
Covid Course 6 (Swahili)
Covid Course 6 (Swahili)
Covid Course 7 (Swahili)
Covid Course 7 (Swahili)
Covid Course 8 (Swahili)
Covid Course 8 (Swahili)

Next Session

Course 1: COVID-19 ni nini?

Course 2: Kinga na Ulinzi

Course 3: Kushughulikia Afya ya Akili na Uzima

Course 4: Muhtasari wa Kutafuta Waliotagusana

Covid Course 5 (Swahili)

Covid Course 6 (Swahili)

Covid Course 7 (Swahili)

Covid Course 8 (Swahili)